Yanga imepania ushindi Algeria

Joel JJ By Joel JJ β€’ 5th December 2024

Yanga imepania ushindi Algeria

Baada ya kikosi kutua salama Algiers jana, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema hawana wasiwasi wowote kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji MC Alger utakaochezwa Jumamosi uwanja wa July 05 1962

Yanga itashuka katika mechi hiyo ya pili ya hatua ya makundi ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-0 na Al Hilal ya Sudan, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam wiki iliyopita

Kamwe amesema kikosi kimewasili salama na kila mchezaji yuko katika hali nzuri kwa ajili ya kuipambania timu

Kamwe amebainisha kuwa watakuwa na takribani siku mbili za maandalizi wakiwa Argeria chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic

"Tunashukuru timu imewasili salama hapa Algiers, tulipata changamoto kidogo ya kuchelewa kutoka uwanja wa ndege baada ya kutua kutokana na taratibu za Kimataifa lakini kila kitu sasa kinakwenda vizuri," alisema Kamwe

Mechi dhidi ya MC Alger itachezwa kwenye Uwanja wa Julai 5, 1962 baada ya maombi ya kuhamishiwa kwenye Uwanja wa Ali la Pointe kukataliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF)

MC Algers ilitaka kupeleka mchezo huo katika Mji wa Douera uliopo kilomita 19 kutoka jijini Algers. Taarifa kutoka CAF zimethibitisha mchezo huo utachezwa kwenye uwanja uliopangwa na kupitishwa na CAF awali

CAF imewafungia MC Algers kucheza michezo minne bila mashabiki kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu yaliyoonyeshwa na mashabiki wao katika mechi ya mwisho ya kufuzu hatua hiyo ya makundi waliyocheza dhidi ya US Monastir ya Tunisia

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’