Klabu ya Pamba Jiji imekamilisha usajili wa beki mkongwe Kelvin Yondani 'Cotton', imefahamika
Yondani ametua Pamba Jiji akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na Geita Gold iliyoshuka daraja msimu uliopita
Yondani hakuwa na timu tangu msimu uliopita kumalizika na sasa anakwenda kuungana na kocha wake wa zamani Fred Felix Minziro waliyefanya nae kazi kwa mafanikio kunako klabu ya Geita Gold misimu miwili nyuma
Yondani ataanza kuitumikia Pamba Jiji baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa Disemba 16



