Ramovic anataka ushindi Algeria

Joel JJ By Joel JJ β€’ 6th December 2024


Ramovic anataka ushindi Algeria

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa July 05 1962

Akizungumza katika mkutano na wanahabari, Ramovic amesema anatambua mchezo huo utakuwa mgumu kwani wanakwenda kucheza dhidi ya timu ngumu lakini anaamini katika ubora wa timu yake na ana imani watafanya vizuri katika mchezo huo

Ramovic amesema Yanga ina historia katika uwanja wa July 05, hivyo kesho itakuwa siku nyingine kwao kusaka ushindi

"Tunakwenda kucheza na timu ngumu, ina wachezaji bora na kocha mzoefu lakini upande wetu tuna kikosi chenye wachezaji bora sana, naamini itakuwa mechi nzuri yenye kuvutia"

"Yanga wana historia kwenye uwanja tutakaotumia kesho, walipoteza mchezo wa Fainali hapa kwa kanuni lakini naamini walishinda mioyo ya wapenda mpira hapa Algeria, kesho ni siku nyingine na tutakuja na nguvu nyingine ya kutaka kushinda mchezo," alisema Ramovic

Kocha huyo raia wa Ujerumani ameongeza kuwa kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Al Hilal kumewaongezea morali katika maandalizi ya mchezo wa kesho ambao wanahitaji kushinda

"Tuko kwenye presha baada ya kupoteza mchezo wa kwanza, lakini imetupa nguvu ya kujiandaa vizuri kuelekea mchezo wa kesho"

"Tumekuja mapema kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa. Hatuwezi kupanga matokeo ya mwisho yatakavyokuwa Lakini tunaweza kupanga jinsi tutakavyocheza ili kupata matokeo mazuri"

"Sio nzuri kucheza mechi bila mashabiki, binafsi napenda kuiona timu yangu ikicheza mbele ya mashabiki wengi, lakini kwa kesho tutawakosa mashabiki hapa uwanjani hivyo tuna jukumu la kupambana kuwapa furaha mashabiki wetu watakaokuwa nyumbani," alisema

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, Stephane Aziz Ki amesema wamejifunza kutoka kile kilichotokea katika mechi mbili zilizopita, kesho wanakwenda kupambana kusahihisha makosa

"Kila siku mpya uwanjani inatupa nafasi wachezaji ya kujifunza kitu kipya, mechi mbili zilizopita, ya Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu zimetupa funzo na kesho tutakwenda kupambana ili tupate matokeo mazuri," alisema Aziz Ki


  

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’