Local,Normal News,CHAN

VAR kutumika michuano ya CHAN

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Dec 2024
VAR kutumika michuano ya CHAN

Katika hatua ya kihistoria kwa soka la ukanda wa Afrika Mashariki, imetangazwa kuwa Teknolojia ya Video Assistant Referee (VAR) itatumika rasmi katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) ya mwakani

Tangazo hili linakuja siku chache kabla ya mashindano hayo, ambayo yatafanyika kuanzia Februari 1 hadi 28, 2025. Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa matumizi ya teknolojia hii, ambayo imekuwa ikitumika katika mashindano makubwa kama vile Ligi ya Mabingwa ya Afrika tangu nusu fainali za mwaka 2021, na pia katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2023

Awali VAR ilishuhudiwa katika fainali za Kombe la Mataifa kwa Vijana U17 zilizofanyika mwaka 2019 kwenye Uwanja wa Azam Complex. Uwanja wa Benjamini Mkapa kwa Tanzania Bara na Amaan huko Zanzibar vitakuwa na mfumo wa VAR, huku vifaa vya teknolojia hii vikitarajiwa kuwasili karibuni ili kuwekewa maandalizi ya mwisho kabla ya mashindano kuanza

Viwanja vingine ambavyo navyo vinatarajiwa kuwekewa mfumo huo mbali na hivyo vya Tanzania ni pamoja na Namboole nchini Uganda, Nyayo na Kasarani nchini Kenya

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki kuwa wenyeji wa michuano hiyo kwa pamoja. Akiongelea hilo, Meneja wa CAF kwa mashindano ya CHAN, Serge Assume alisema kuwa vifaa vya VAR vitakamilishwa na kufanyiwa majaribio kabla ya michuano kuanza

Teknolojia ya VAR itasaidia kuboresha ubora wa uamuzi wa waamuzi, hasa katika hali zinazohitaji uamuzi wa haraka na sahihi

Inatumika katika masuala manne makuu ya mchezo, ambayo ni Uamuzi wa goli, uamuzi wa penalti, kadi nyekundu za moja kwa moja, kufichua makosa

Teknolojia ya VAR inajumuisha vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na kamera zinazochukua mechi kutoka mikao mbalimbali, msaidizi wa VAR anayefuatilia mchezo, msaada wa waamuzi wa VAR, Opereta wa kurejesha video, eneo la mapitio ya waamuzi (RRA), ambapo waamuzi wataweza kupitia uamuzi wao, VAR Light na VHF Omnidirectional Range, ambavyo vinatuma ishara kutoka kituo cha ardhini hadi kwenye antena ya mfumo

Mwanaspoti

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
14m ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
3h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
5h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
7h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
9h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
10h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
10h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
12h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
15h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
23h ago
READ MORE β†’