Wakati kikosi cha Simba kikiwa Algeria kwa ajili ya mchezo wa pili wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho dhidi ya CS Constantine, kiungo mshanbuliaji Elie Mpanzu ameendelea kujifua takribani wiki moja na siku kadhaa zikiwa zimesalia kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa
Disemba 18 Mpanzu anaweza kuanza kuitumikia Simba katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Ken Gold
Nyota huyo aliyesajiliwa na Simba akitokea klabu ya AS Vita ya DR Congo, anasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa timu hiyo
Mpanzu anafanya mazoezi na Simba tangu mwezi Septemba, ni wazi hatahitaji muda kuonyesha ubora wake kwani kazi hiyo tayari inaelezwa anaifanya katika kiwanja cha mazoezi
Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids mara kadhaa amesikika akisifu usajili wa winga huyo akidai ni mchezaji anayeingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza
Simba pia inatarajiwa kumuongeza Mpanzu katika kikosi chake cha CAF na pengine anaweza kutumika katika mechi tatu za mwisho kuhitimisha hatua ya makundi