Yanga yapoteza tena Algeria

Joel JJ By Joel JJ β€’ 8th December 2024

Yanga yapoteza tena Algeria

Yanga imeacha alama nyingine tatu Algeria baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya MC Alger

Vijana wa kocha Saed Ramovic walicheza kwa nidhamu kubwa kwenye kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko bila kuruhusu bao

Hata hivyo mambo hayakuwa mazuri upande wao katika kipindi cha pili baada Ayoub Abdelloui akifunga kwa kichwa dakika ya 64 baada ya walinzi wa Yanga kuzembea kuondoa mpira wa adhabu

Kuingia kwa bao hilo ni kama kuliiamsha Yanga iliyoanza kupeleka mashambulizi langoni kwa MC Alger lakini bado Alger waliendelea kuwa hatari kupitia mashambulizi ya kushitukiza

Mlinda lango Djigui Diarra akafanya makosa dakika za lala salama baada ya kutokea mpira ambao hakufanikiwa kuucheza na kuwapa nafasi Alger kufunga bao la pili

Ni alama nyingine tatu zinapotea ikiwa mechi ya pili Yanga inapoteza katika michuano ya ligi ya mabingwa

Mchezo unaofuata Yanga inakwenda tena ugenini kumenyana na TP Mazembe, Disemba 14

Bado kimahesabu Yanga ina nafasi ya kufanya vizuri ikiwa itashinda mechi mbili zilizobaki nyumbani na pia kufanya vizuri katika mechi nyingine mbili zilizobaki ugenini dhidi ya TP Mazembe na Al Hilal

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’