International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Disemba 09 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Dec 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Disemba 09 2024

Klabu tatu za ligi ya Premier bado zinavutiwa na Dusan Vlahovic, Liverpool watoa ofa ya kwanza kwa Mohamed Salah na pia wanataka Virgil van Dijk na Trent Alexander-Arnold kusaini mikataba mipya

Arsenal, Chelsea na Manchester United bado wanavutiwa na Dusan Vlahovic, huku Juventus wakifikiria kumuuza mshambuliaji huyo wa Serbia, 24, isipokuwa kama atakubali mkataba mpya. (TBR Football)

Liverpool wametoa ofa ya mkataba mpya wa mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 32. (Athletic – Subscription Required)

Liverpool pia wanatazamia kuwafunga beki wa kati wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33, na mlinzi wa kulia wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, kwa mikataba mipya. (Star)

Manchester City wanaweza kuharakisha kuipiku Liverpool katika mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Martin Zubimendi, 25, kutoka Real Sociedad. (Football Insider)

Jitihada za Crystal Palace kumsajili winga wa Lyon Mfaransa Rayan Cherki mwenye umri wa miaka 21 zimezuiliwa na wababe wa Ulaya Paris St-Germain pamoja na Borussia Dortmund wanaojiunga katika kinyang'anyiro hicho. Sun)

Aston Villa ni moja kati ya klabu nne za Ligi Kuu ya Uingereza zinazomtaka winga wa Juventus na Uturuki Kenan Yildiz, 19, ambaye klabu yake inawweza kumuuza kwa takriban £66m. (BirminghamLive, nje)

AC Milan wana nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea Muingereza Carney Chukwuemeka, 21, ambaye pia anawavutia Celtic kwa mkopo. (Soccer Italia)

Mshambulizi wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 18, Endrick ameamua kutoondoka kwa mkopo mwezi Januari na ataendelea kupigania nafasi ya kuanzishwa. (Marca – In Spanish)

Winga wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 23, anakaribia kusaini mkataba wa nyongeza na Napoli hadi 2029. (Corriere dello Sport – In Itali)

West Ham ilimchukulia Massimiliano Allegri kama mrithi wa kocha wa sasa Julen Lopetegui lakini gharama inayohusika inafanya uwezekano wa kutoanza. (Football Insider)

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
8h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
11h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
13h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
15h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
17h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
18h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
18h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
20h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
23h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’