Yanga kuvuta kiungo Singida BS

Joel JJ By Joel JJ β€’ 9th December 2024

Yanga kuvuta kiungo Singida BS

Wakati zimebaki siku sita tu kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa, Klabu ya Yanga ipo kwenye hatua za mwisho kupata saini ya kiungo mkabaji wa Singida Black Stars, Kelvin Nashon, imefahamika

Habari kutoka ndani ya Yanga, zinasema kuwa mchezaji huyo ana asilimia kubwa ya kujiunga na Yanga kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita

Nashon anatarajiwa kutua kuongeza nguvu kusaidiana na Khalid Aucho ambaye kwa sasa amekuwa akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara, akicheza pia mechi nyingi ambazo zimeonekana kuathiri kiwango chake

"Nadhani Nashon anaweza kutusaidia kwa sasa, tutamchukua kwa mkataba wa muda mfupi wa miezi sita, kama akifanya vizuri, basi mwishoni mwa msimu tutakaa na Singida Black Stars kwa ajili ya kufanya biashara nyingine, kwani tutamsajili kwa miaka miwili"

"Angalia hivi sasa kocha wetu, Sead Ramovic, ameamua kumchezesha Duke Abuya namba sita, wakati ni winga na kiungo mshambuliaji, kwa sababu tuna mapungufu kidogo kwenye eneo hilo, tunachohitaji ni ubora na Nashon timu zote alizoenda ameonekana yupo imara na kiwango chake hakishuki," alisema mtoa taarifa

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’