Kocha Mkuu wa klab ya Pamba jiji Fred Felix Minziro ameanza taratibu kuitoa pamba Jiji kule bondeni kuelekea nafasi ambazo zinaweza kuwapa uhakika wa kuendelea kubaki ligi kuu msimu ujao
Pamba walianza vibaya msimu chini ya Kocha Goran Kopunovic, lakini baada Minziro kukabidhiwa timu hiyo, mabadiliko yanaonekana
Mpaka sasa Pamba jiji ipo nafasi ya 12 na alama zao 11 baada ya kucheza michezo 13 ambapo wameshinda michezo 2,Kupoteza 6 na sare 5
Minziro anasifika kwa uwezo wake wa kusaidia timu kupanda daraja zinapokuwa daraja la kwanza kwenda ligi Kuu kwani amefanya hivyo kwa timu kadhaa pia ni bingwa wa kuziokoa timu zinapokuwa na nyakati ngumu
Amefanya hivyo kwa timu kadhaa mfano mzuri ni msimu uliopita alipoipokea Kagera Sugar na kumaliza ndani ya 10 bora



