Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa (CAF CL) Yanga wana kazi ya kufanya ili kuweza kutinga robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuanza hatua ya makundi kwa kusuasua
Baada ya juzi kupoteza mchezo wa pili mfululizo kwa kufungwa mabao 2-0 na MC Alger, Yanga imeendelea kushika nafasi ya nne kundi A ikiwa haina pointi
Vinara wa kundi hilo Al Hilal jana walipata ushindi mwingine wa mabao 2-1 dhidi ya TP Mazembe na hivyo kufikisha alama 6
MC Alger wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama nne huku TP Mazembe wakiwa wa tatu na alama 1
Kila timu imesalia na mechi nne, hivyo licha kutokuwa na pointi mpaka sasa bado Yanga ina nafasi ya kusonga mbele hatua inayofuata kama itafanya vizuri katika mechi hizo zilizobaki
Mechi mbili dhidi ya TP Mazembe na MC Alger watacheza nyumbani huku mechi nyingine mbili dhidi ya Mazembe na Al Hilal watacheza ugenini
Mchezo unaofuata Yanga itasafiri Lubumbashi DR Congo kuikabili Mazembe kabla ya timu hizo kurudiana wiki mbili baadae jijini Dar es salaam
Yanga inahitaji kushinda angalau mechi tatu ili kuwa na nafasi ya kutinga robo fainali



