International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Disemba 10 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Dec 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Disemba 10 2024

Mshambulizi wa Uingereza Cole Palmer, 22, anaivutia Real Madrid kwa sababu ya mchezo wake thabiti akiwa Chelsea. (Fichajes - Spanish)

West Ham itaongeza nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, dirisha la uhamisho la Januari litakapofunguliwa. (Football Insider)

Arsenal, Manchester United na Barcelona wako tayari kupigana vikumbo kwa ajili ya kumnasa fowadi wa Lille kutoka Canada Jonathan David, 24, ambaye kandarasi yake inamalizika msimu wa joto. (Mundo Deportivo - Spanish)

Manchester City wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Norway Oscar Bobb, 21, au kiungo wa kati wa Uingereza James McAtee, 22, huku wakitafuta kuwashawishi Bayer Leverkusen kuachana na winga wao wa miaka 21 wa Ujerumani Florian Wirtz. (TBR Football)

Meneja wa Manchester United Ruben Amorim anaweza kuwatoa kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 32, na winga wa Brazil Antony, 24, ili kuokoa pesa mwezi Januari. (GiveMeSport)

Liverpool wanatumai kuwashinda wapinzani kadhaa wa Uropa kuinasa saini ya beki wa Bologna Mholanzi Sam Beukema, 26. (Teamtalk)

Kiungo wa kati wa Motherwell na Scotland Lennon Miller, 18, pia analengwa na Liverpool na anaweza kupatikana kwa £8m. (Caught Offside)

Beto wa Everton, 26, anaweza kurejea Italia mwezi Januari, huku Torino ikimtaka mshambuliaji huyo wa Guinea-Bissau. (Tuttomercartoweb - In Itali )

Mchezaji wa Atalanta Ademola Lookman, 27, yuko tayari kurejea Uingereza, huku klabu kadhaa za Ligi ya Premia zikimtaka fowadi huyo wa Nigeria. (GiveMeSport)

Chelsea itamtuma kiungo wa kati wa Uingereza Omari Kellyman kwa mkopo mwezi Januari ili kumsaidia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 kupata uzoefu wa juu. (Football Insider)

Graham Potter yuko tayari kuchukua kazi ya West Ham mwanzoni hadi mwisho wa msimu, ikiwa watamfuta kazi Julen Lopetegui. (Sportsport)

Tottenham wanatazamiwa kumuunga mkono meneja Ange Postecoglou na kumsaidia raia huyo wa Australia katika dirisha dogo la usajili la Januari, licha ya matokeo mabaya.(Teamtalk)

Manchester United huenda wakapanga vita dhidi ya Arsenal kumnunua Luis Campos, mshauri wa soka wa Paris St-Germain. (ipaper)

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
2h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
6h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
12h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
12h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
12h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
18h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’