Local,Normal News,Simba

Simba yaweka hadharani viingilio mchezo dhidi ya CS Sfaxien

Joel JJ By Joel JJ
10 Dec 2024
Simba yaweka hadharani viingilio mchezo dhidi ya CS Sfaxien

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali ametangaza viingilio vya mchezo wa tatu wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho (CAF CC)  dhidi ya CS Sfaxien ambao utapigwa Jumapili, Disemba 15 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Ili kuhakikisha Wanasimba wengi wanajitokeza uwanja wa Benjamin Mkapa kuishangilia timu yao, Ahmed amesema uongozi umepunguza bei ya viingilio ambapo majukwaa pendwa ya Mzunguuko kiingilio ni Tsh 3,000/-

  • Tanzanite - Tsh. 250,000
  • Platinum - Tsh. 150,000
  • VIP A - Tsh. 30,000
  • VIP B - Tsh. 20,000
  • VIP C - Tsh. 10,000
  • Machungwa - Tsh. 5,000
  • Mzunguko - Tsh. 3,000

Aidha Ahmed amesema lengo ni kuhakikisha wanakwenda kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa na kuipa hamasa Simba katika mchezo ambao alama tatu lazima zbaki nyumbani

"Tarehe 15 siku ya Jumapili saa 10:00 jioni kunako Uwanja wa Mkapa ni siku ya kumuangamiza CS Sfaxien. Na hili halitawezekana kwa Fadlu peke yake, kwa Camara peke yake bali kwa Wanasimba wote kuja uwanjani, hakuna Mwanasimba anayetakiwa kubaki nyumbani. Kama kweli tuna nia ya kumuangamiza mpinzani wetu basi hatuna budi aache nyumba yake aje Benjamin Mkapa."

"Kila kiongozi wa tawi, kila kiongozi wa kundi ana jukumu la kuhimiza Wanasimba wenzake kuja uwanjani. Hakuna sababu yoyote ya Mwanasimba kubaki nyumbani. Utaipendaje Simba kama huifati ilipo?"

"Kupoteza na CS Constantine kusitutoe kwenye reli, nafasi yetu ya kwenda robo fainali bado nyeupe kabisa. Nafasi yetu bado iko wazi tukifanya vizuri mechi inayofata."

"Baada ya kupoteza mchezo wa juzi kuna wenzetu wakaanza kukata tamaa lakini niwambie tu tuko salama sana, hakuna kilichobadilika, nafasi yetu ya kwenda robo fainali iko palepale. Niwakumbushe msimu juzi mpaka mchezo wa pili hatukuwa na alama yoyote na tukaibukia kwa Vipers na kila mmoja anakumbuka Mnyama akavuka kwenda robo fainali."

"Mchezo wa Jumapili lazima kila Mwanasimba ajue umuhimu wake maana mpinzani tunayekutana nae anataka kufufukia kwetu na sisi hatuko tayari kuona CS Sfaxien anafufukia kwetu. Hakuna ambaye amewahi kupata uhai ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa."

"Kwa kuwa mechi hii tunataka tuwe na mashabiki wengi Benjamin Mkapa, tunataka kujaza Benjamin Mkapa. Mara ya mwisho kujaza Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Simba Day. Tumeamua kuweka viingilio ambavyo havitampa mtu sababu ya kutokuja uwanjani lakini pia tupo karibu na sikukuu za mwaka. Na sisi tumeamua kupunguza viingilio ili kila Mwanasimba aje uwanjani," alisema Ahmed

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
7h ago
READ MORE →
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
11h ago
READ MORE →
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
12h ago
READ MORE →
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
14h ago
READ MORE →
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE →
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
17h ago
READ MORE →
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
17h ago
READ MORE →
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
19h ago
READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
22h ago
READ MORE →
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE →