Yanga yamtambulisha Mwenda

Joel JJ By Joel JJ β€’ 11th December 2024


Yanga yamtambulisha Mwenda

Siku tano kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa, Yanga imeanza kutambulisha silaha zake mpya baada ya mabingwa hao wa Tanzania Bara kutambulisha usajili wa mlinzi wa pembeni Israel Mwenda

Mwenda ametua Yanga kwa mkopo wa hadi mwishoni mwa msimu akitokea klabu ya Singida Black Stars

Beki huyo mwenye umri wa miaka 24, anamudu kucheza nafasi zote za ulinzi wa pembeni kulia na kushoto

Kabla ya kusajiliwa na Singida Black Stars mwanzoni mwa msimu huu, Mwenda alizitumikia klabu za KMC na Simba mara kadhaa akipata nafasi ya kuitwa timu ya Taifa

Yanga inakabiliwa na changamoto katika safu ya ulinzi hasa upande wa kushoto ambapo beki tegemeo Chadrack Boka anakabiliwa na majeraha ya mara kwa mara

Mbadala wake Nickson Kibabage hajaonyesha ushawishi wa kutosha kuaminiwa katika nafasi hiyo huku Kibwana Shomari akikosekana kwenye kikosi cha kwanza kwa muda mrefu kwa kilichoelezwa kupungua makali yake


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.