Mpanzu kuongezwa kikosi cha Simba CAF

Joel JJ By Joel JJ β€’ 11th December 2024

Mpanzu kuongezwa kikosi cha Simba CAF

Kiungo mshambuliaji wa Simba Elie Mpanzu ataanza kuwatumikia Wekundu hao wa Msimbazi katika michuano ya kombe la Shirikisho la CAF (CAF CC) baada ya Januari 1 2025

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali ametoa ufafanuzi kuwa dirisha dogo la usajili la CAF litafunguliwa Januari 01 na kufungwa Januari 31 2025 wakati dirisha dogo la TFF likifunguliwa Disemba 16 na kufungwa Januari 15 2025

Hivyo Mpanzu ataanza kuitumikia Simba kwenye ligi ya ndani kuanzia wiki ijayo baada dirisha la TFF kufunguliwa lakini atalazimika kusubiri Januari 1 ili asajiliwe katika kikosi cha Simba kinachoshiriki kombe la Shirikisho

"Disemba 15 litafunguliwa dirisha ndogo la usajili wa ndani na Ellie Mpanzu atasajiliwa hapo kwa maana hiyo mechi yoyote ya ndani baada ya tarehe 15 atakuwa sehemu ya kikosi lakini dirisha la CAF ni mpaka Januari, 2025 kwahiyo mechi yoyote ya kimataifa kuanzia Januari atakuwa sehemu ya kikosi," alisema Ahmed

Disemba 18 Simba itacheza mechi ya ligi kuu dhidi ya KenGold ambayo itapigwa uwanja wa KMC Complex, huenda ikawa mechi ya kwanza kwa Mpanzu kuitumikia Simba

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’