Simba dimbani dhidi ya CS Sfaxien CAF CC leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 15th December 2024

Simba dimbani dhidi ya CS Sfaxien CAF CC leo

Mikiki mikiki ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) inaendelea leo ambapo Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc watakuwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili CS Sfaxien kutoka Tunisia

Mechi muhimu kwa Simba kubeba alama zote tatu leo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya robo fainali

Simba inayoshika nafasi ya pili kundi A, ilipoteza mchezo uliopita dhidi ya CS Constantine uliopigwa Algeria, leo ni matokeo ya aina moja tu ambayo mashabiki wa Simba wanayatarajia, USHINDI

Licha ya kupoteza mechi zao mbili, CS Sfaxien sio timu nyepesi na bila shaka leo huenda wakatoa upinzani mkali kwa Simba

Timu hiyo ilitua nchini mapema ambapo wako katika ardhi ya Tanzania kwa takribani siku sita

Walisafiri moja kwa moja kutoka Angola kuja Tanzania baada ya mchezo dhidi ya Bravos ambao walipoteza kwa mabao 3-2 Jumapili iliyopita

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema leo vijana wake watakuwa tofauti kimbinu ukilinganisha na mechi yao iliyopita ambayo walikuwa ugenini

Simba leo inatarajiwa kucheza soka la kushambulia zaidi huku wakichukua tahadhari ya mashambulizi ya kushitukiza ya Sfaxien

Mchezo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 10 jioni..

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’