Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Palamagamba Kabudi amesikitishwa na vitendo vya mashabiki kung’oa viti katika uwanja wa Benjamin Mkapa Siku ya jana katika mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Simba dhidi ya CS Sfaxien
Waziri Kabudi amemuagiza Katibu mkuu wa wizara hiyo kuchukua hatua mara moja kuwaandikia barua Simba na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili gharama za uharibifu zilizosababishwa wakati wa wa mechi hiyo zilipwe
Aidha klabu ya Simba imetakiwa kutoa Ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili wote waliong’oa viti wakamatwe na wachukuliwe hatua za kisheria ili kukomesha tabia hiyo
