Rupia awaita Simba mezani

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Dec 2024
Rupia awaita Simba mezani

Kinara wa mabao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Elvis Rupia, amesema atakuwa tayari kujiunga na Simba kama kweli wanamhitaji na watapitia kwenye njia sahihi za kuongea na klabu yake ya Singida Black Stars, kwani hakuna mchezaji yeyote nchini ambaye hataki kuichezea timu hiyo

Rupia, raia wa Kenya, alisema hayo juzi kutokana na tetesi kuwa Klabu ya Simba inataka saini yake kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili

"Mpaka sasa binafsi sijapata ofa kutoka klabu yeyote, labda inaweza kuja baadaye, ukweli hakuna mchezaji yeyote nchini ambayo haipendi kucheza Simba au Yanga, ikitokea ofa na nikakubaliana nayo naweza kwenda," alisema mchezaji huyo

Habari kutoka ndani ya Klabu ya Simba zinasema kuwa inamhitaji mchezaji huyo kwa ajili kuongeza nguvu kwenye kikosi cha timu hiyo nafasi ya ushambuliaji ambayo ina Leonel Ateba, Steven Mukwala na Valentino Mashaka

Hata hivyo, wakati Simba ikionesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo, habari zinasema kuwa Yanga nayo ina mpango wa kupiga hodi kwenye klabu hiyo kuulizia huduma ya mchezaji huyo ambaye amefikisha jumla ya mabao saba ya kufunga kwenye Ligi Kuu, akimpiku straika wa Fountain Gate, Selemani Mwalimu, aliyeongoza kwa muda mrefu akisalia na mabao sita

Akizungumzia siri ya kupachika mabao, Rupia alisema ni kufanya mazoezi kwa bidii na amejiwekea malengo ya kufunga bao moja katika kila mechi, ingawa baadhi ya michezo ameshindwa kufanya hivyo

"Kulingana na jinsi ninavyofanya mazoezi, nimekuwa nikijiwekea malengo angalau nifunge bao moja kila mchezo, ila kuna wakati haitokei, nashukuru kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji nilifunga mabao yote mawili nikaipa ushindi timu yangu ya mabao 2-1, sikujua kama nitafunga mawili, moja limeongezeka"

"Ni furaha sana kwa sababu kila straika anataka kuwa hapo juu, kila mmoja anapambana anavyoweza aweze kufika hapo. Binafsi natarajia kuendelea kufunga mabao mengi, huko mbele ndiyo tutajua ni nani atakuwa mfungaji bora," alisema Rupia

IPP Media

ADVERTISE HERE

More Stories

Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
24m ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
1h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
1h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
4h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
6h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
7h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
7h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
9h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
10h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
10h ago
READ MORE β†’