Klabu ya Singida Black Stars imeachana na mshambuliaji raia wa Ivory Coast Joseph Guede
Guede alijiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia Yanga kwa miezi sita
Hata hivyo ameshindwa kuonyesha makali yake kwa walima alizeti hao na hatimaye jana Singida BS wakatoa taarifa ya kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake
"Tumefikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na aliyekuwa mchezaji wetu katika safu ya ushambuliaji, Joseph Gnadou Guede. Uongozi wa Klabu unamshukuru Guede kwa kipindi chote alichoitumikia timu yetu na tunamtakia kila la kheri katika safari yake ya soka," ilisema taarifa ya Singida BS
Guede amewahi kutamba katika klabu za RS Berkane na FAR Rabat zote za Morocco
ADVERTISE HERE