Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi za raundi ya 15 zitaendelea katika viwanja viwili
Walina asali Tabora United watakuwa dimba la Ali Hassan Mwinyi kuikaribisha Coastal Union katika mchezo utakaopigwa saa 10 jioni
Tabora United wamekuja na utaratibu wa 'kurambisha' asali kila anayekanyaga dimba la Ali Hassan Mwinyi, je wataendeleza utaratibu huo mbele ya Coastal Union leo?
Azam Fc baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Tabora United, watakuwa na nafasi ya kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi pale watakapowakaribisha Fountain Gate dimba la Azam Complex, mchezo utakaopigwa saa 1 usiku




