Kocha Simba apania ushindi dhidi ya KenGold

Joel JJ By Joel JJ β€’ 17th December 2024

Kocha Simba apania ushindi dhidi ya KenGold

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema licha ya ugumu wa ratiba inayowakabili mbele yao, kikosi chake kiko tayari kuwania alama tatu katika mchezo unaofuata ligi kuu ya NBC dhidi ya KenGold

Baada ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya CS Sfaxien ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, kesho tena Simba inashuka dimba la KMC Complex kuikabili KenGoldΒ 

Fadlu amesema baada ya kuwapa mapumziko wachezaji wake hapo jana, leo watakamilisha maandalizi kuelekea mchezo huo ambao wanazihitaji alama zote tatu

Fadlu amesema hawapaswi kuwadharau wapinzani wao licha ya nafasi waliyopo katika msimamo wa ligi kwani hawana cha kupoteza

"Tunakabiliwa naa ratiba ya kucheza mechi nne ndani ya muda mfupi lakini lazima tuwe tayari kwa ratiba hii"

"Baada ya mchezo dhidi ya CS Sfaxien, leo tutafanya maandalizi yetu ya mwisho kwa kuzingatia aina ya mpinzani tunayekwenda kucheza nae"

"Tunajua ubora wa KenGold, tunapaswa kucheza kwa tahadhari bila kuwapa nafasi ya kutushambulia kwa kushitukiza"

"Haitakuwa mechi nyepesi hivyo hatupaswi kufikiria tutakwenda uwanjani na kuchukua alama tatu tu, tutahitaji kupambana na muhimu zaidi ni kushinda mchezo huo", alisema Fadlu

Katika kipindi cha siku 10 Simba inatarajiwa kucheza mechi nne za ligi kuu. Mchezo utakaofuata baada ya KenGold ni dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Disemba 21 uwanja wa Kaitaba, Kagera

Baada ya mchezo huo, Simba itarejea Dar kumenyana na JKT Tanzania Disemba 24 kisha kusafiri mkoani Singida kuikabili Singida BS, Disemba 28

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’