Nyota wa Real Madrid, Vini Jr jana alitawazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa FIFA kwa upande wa Wanaume huku Aitana Bonmati akishinda tuzo hiyo kwa upande wa wanawake
Vinicius mwenye umri wa miaka 24 alisikitishwa sana na kushindwa na kiungo wa kati wa Manchester City Rodri kwa tuzo ya Ballon d'Or mwezi Oktoba na kupelekea yeye na timu yake ya Madrid walipuuza sherehe hizo mjini Paris
Wakati huu, Rodri alimaliza wa pili kwa Vinicius kwa alama tano. Fowadi huyo wa Brazil alikuwa kwenye hafla ya FIFA ya kuchukua tuzo yake, baada ya kusafiri hadi Doha Jumatatu na Madrid kwa fainali ya Kombe la Mabara dhidi ya Pachuca
"Sijui hata nianzie wapi," Vinicius alisema kwa Kireno. Nilikuwa mbali sana hivi kwamba ilionekana kuwa haiwezekani kufika hapa. Nilikuwa mtoto ambaye alicheza soka bila viatu tu kwenye mitaa ya Sao Goncalo, karibu na umaskini na uhalifu"
"Kufika hapa ni jambo muhimu sana kwangu. Ninafanya hivyo kwa ajili ya watoto wengi wanaofikiri kwamba kila kitu hakiwezekani na wanaofikiri hawawezi kufika hapa"
Tuzo ya golikipa bora ilikwenda kwa Emiliano Martinez huku Carlo Ancelloti kocha wa Real Madrid akibeba tuzo ya kocha bora wa mwaka