Klabu ya Tanzania Prisons imemfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mbwana Makata na aliyekuwa Kocha Msaidizi wake
Ni kutokana na mfululizo wa matokeo yasiyo ridhisha ikitoka kuchapwa mabao 2-0 na Singida Black Stars na kushuka hadi nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi yenye timu 16
Kwa sasa timu hiyo iko chini ya Kaimu Kocha Mkuu Shaban Kazumba na Msaidizi wake Shaban Mtupa.
Mchezo unaofuata kwa Tanzania Prisons ni dhidi ya Yanga ambao utapigwa Disemba 22 katika uwanja wa KMC Complex
Prisons inatarajiwa kuondoka Mbeya leo kuelekea Dar es salaam tayari kwa mchezo huo