Morrison matatani, aitwa Polisi kwa mahojiano

Joel JJ By Joel JJ β€’ 19th December 2024


Morrison matatani, aitwa Polisi kwa mahojiano

Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi baada ya aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Simba, Bernard Morrison, kulituhumu jeshi hilo kituo cha Mbweni kuwa linachukua rushwa, likimtaka staa huyo kufikia kituo hapo

Juzi Morrison raia wa Ghana, alisambaza taarifa katika mitandao ya kijamii akikituhumu kituo cha Polisi Mbweni kuwa Polisi wake wanachukua rushwa na wanafanya kazi kwa maslahi yao binafsi

"Kuna watu wanafanya kazi kwenye kituo cha Mbweni hawasaidii watu wenye shida na wana maslahi yao binafsi, wanajichukulia sheria mkononi na kufanya wanavyotaka, ikiwa mimi ninayejua vizuri ninaweza kutapeliwa na kutoheshimiwa unafikiri wananchi wa kawaida wanaweza kufanyaje," ilisema taarifa ya Morrison

Hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia taarifa iliyotolewa leo kupitia na Msemaji wake David Misime imesema kuwa Morrison anatakiwa kusema ukweli

Mwanaspoti


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.