Local,Normal News,Simba, Kagera

Fadlu apania ushindi wa kwanza Kaitaba

Joel JJ By Joel JJ
20 Dec 2024
Fadlu apania ushindi wa kwanza Kaitaba

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema kikosi chake kimetua mkoani Kagera kikiwa kamili  kwa lengo la kubeba alama zote tatu katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa uwanja wa Kaitaba kesho Jumamosi

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Fadlu amesema misimu ya karibuni Simba haijapata ushindi katika uwanja wa Kaitba lakini sasa ni wakati wa kubadilisha rekodi hiyo

"Tumekuja hapa tukiwa na dhamira moja, kusaka ushindi katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar"

"Rekodi zinaonyesha hatua matokeo mazuri dhidi ya wapinzani wetu hasa wanapokuwa nyumbani katika misimu kadhaa iliyopita"

"Awamu hii tumekuja kivingine na maandalizi tuliyoyafanya tunaamini tutapata ushindi," alisema Fadlu

Katika misimu miwili ya 2022/23 na 2023/24 Simba iliondoka na alama moja Kaitaba ikilazimishwa sare ya bao 1-1 katika mechi zote mbili

Msimu huu mpaka sasa Simba imeweka rekodi ya kibabe katika mechi za ugenini, wakibeba alama tatu katika kila mechi

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
45m ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE →
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE →
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE →
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE →
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE →
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE →
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE →