Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mchezo mmoja utapigwa uwanja wa KMC Complex, Kinondoni jijini Dar es salaam
Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga watakuwa na kibarua kizito mbele ya Tanzania Prisons katika mchezo utakaopigwa saa jioni
Ni mechi itakayokutanisha timu mbili zenye malengo tofauti. Yanga itakuwa ikisaka ushindi mnono ili isogee katika nafasi ya pili kwenye msimamo na kuendelea kuwapa presha watani zao Simba ambao jana walipata ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Kagera Sugar
Tanzania Prisons imekusanya alama 11 katika mechi 14 ikishika nafasi ya 14, ni wazi watashuka katika dimba la KMC Complex leo kupambana kujiondoa katika eneo la hatari
Utakuwa mchezo wa tatu wa ligi kwa kocha mkuu wa Yanga Sead Ramovic ambaye amekusanya alama 6 kwa timu yake kushinda mechi mbili zilizopita
Aidha utakuwa mchezo wa pili kwa Yanga kucheza katika dimba la KMC Complex baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mashujaa Fc katika uwanja huo mshambuliaji Prince Dube akifungua akaunti yake ya mabao msimu huu akifunga hat-trik
Yanga inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 30, ushindi wa kuanzia mabao matatu utawahakikishia Wananchi kusogea katika nafasi ya pili
