Uongozi wa Simba umepokea barua ya ombi la kuvunja mkataba kutoka kwa mlinda lango Aishi Manula ambaye amepoteza nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo
Taarifa za ndani zimethibitisha kuwa Manula ameandika barua ya kuomba kuvunja mkataba wake wa miezi sita uliobaki ili akatafute changamoto sehemu nyingine
Aidha presha ni kubwa kwa Simba kwa kuwa Manula ndiye kipa tegemeo wa timu ya Taifa na kutocheza kwake kunaweza kuathiri mipango ya Stars kuelekea fainali za CHAN 2025 zitakazofanyika Februari 2025 na michuano ya Afcon 2025
Kwa sasa Manula hana nafasi katika kikosi cha Simba, Moussa Camara ndiye kipa namba moja akisaidiwa na Ali Salim ambaye ni kipa namba 2
Huenda mlinda lango huyo aliyejijengea heshima kubwa Simba na kuitwa Tanzania One, akaruhusiwa kuondoka katika dirisha hili