Mshambulaji wa Singida Black Stars Elvis Rupia bado yuko kileleni katika mbio za ufungaji bora wakati mechi 15 za duru ya kwanza zikielekea kukamilika
Rupia anaongoza na mabao yake 7 akifuatiwa na Selemani Mwalimu aliyepachika mabao 6 sawa na Jean Ahoua wa Simba ambaye pia amepachika mabao 6
Edgar Willian (Fountain Gate), Peter Lwasa (Kagera Sugar) na Lionel Ateba (Simba) wanafuatia katika orodha hiyo kila mmoja akiwa amefunga mabao 5

Mlinda lango wa Moussa Camara wa Simba anaongoza kwa cleensheet(10), Akifuatiwa na Patrick Munthali wa Mashujaa mwenye cleenshet 8 huku Djigui Diarra akiwa wa tatu na cleensheet 7

Kwa upande wa vinara wa pasi za mabao, Feisal Salum (Azam Fc) ni kinara akitoa pasi 7 akifuatiwa na Salum Kihimbwa (Fountain Gate) aliyetoa pasi 5
Stephane Aziz Ki, Jean Ahoua na Josephat Author kila mmoja ametoa pasi 4 za mabao
