Local,Normal News,

Manara aonywa na Jeshi la Magereza

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Dec 2024
Manara aonywa na Jeshi la Magereza

Jeshi la Magereza Tanzania Bara limemuonya aliyekuwa Msemaji wa Yanga, Haji Manara akituhumiwa kutoa kauli isiyo ya kiungwana juu ya jeshi hilo anayodaiwa kuitoa katika mchezo wa Ligi Kuu kati ya Yanga na Tanzania Prisons uliochezwa jana katika Uwanja wa KMC Complex na Yanga kushinda mabao 4-0

Kupitia taarifa iliyotolewa leo, Desemba 23, 2024 na Msemaji wa jeshi hilo, Kamishna Mwandamizi (SACP), Elizabeth Mbezi, imesema jana Jumapili Desemba 22, 2024 muda mfupi baada ya kumalizika mchezo huo Manara alionekana akibishana na watu wa Magereza waliokuwa wakimuomba asogeze gari lake ili wapitishe la kwao kwani alikuwa ameziba njia

"Jeshi la Magereza Tanzania Bara linapenda kuujulisha umma kuwa limesikitishwa na kauli isiyo ya kiungwana iliyotolewa na Haji Sunday Manara baada ya kumalizika kwa mchezo Na 110, mzunguko wa 14 uliochezwa jana kati ya Young Africans na Tanzania Prisons katika Uwanja wa KMC Complex"

"Baada ya kumalizika kwa mchezo huo Haji Manara alianza kuongea na vyombo vya habari akiwa ameegesha gari lake mbele ya gari la Jeshi la Magereza. Kwa kuwa alikuwa amezuia gari la jeshi kuondoka aliombwa atoe nafasi kwa kusogeza gari lake kuruhusu gari alilokuwa amelizuia liweze kupita na yeye aendelee na mahojiano yake"

"Hata hivyo, pamoja na kuombwa alikataa kwa dharau na kuanza kutoa maneno yasiyo ya kiungwana, yenye viashiria vya kutweza utu na yenye mwelekeo wa kulifedhehesha Jeshi la Magereza"

"Uongozi wa Jeshi unatoa onyo na kuwataka wananchi kuacha kutoa kauli zenye mwelekeo wa kubeza, kutweza, kudharau mamlaka yake au kulifedhehesha na kwamba halitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayehusika," ilibainisha taarfa ya Jeshi la Magereza

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
1m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
30m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’