Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi mbili zinatarajiwa kupigwa
Mchezo wa mapema saa 8 utapigwa uwanja wa CCM Liti ambapo Singida Black Stars watakuwa wenyeji wa vibonde KenGold
Ushindi kwa Singida BS utawahakikishia walima alizeti hao kufikisha alama 33 na kuwa sawa na Yanga na Azam Fc zilizo juu yao
Singida BS walio nafasi ya nne katika msimamo, watahitaji ushindi wa zaidi ya mabao 4 ili kuiondoa Azam Fc katika nafasi ya tatu
Mambo bado ni magumu upande w KenGold ambao wamekusanya alama 6 kutoka mechi 14
Matokeo ya ushindi kwao hayawezi kuwaondoa mkiani lakini yatapunguza gap la pointi dhidi ya timu zilizo juu yake
Vinara wa ligi hiyo Simba watachuana na JKT Tanzania katika mchezo mwingine utakaopigwa saa 10 jioni
Ushindi kwa Simba utawahakikishia kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi kabla ya mchezo wao dhidi ya Singida BS utakaopigwa Disemba 28 huko Singida
JKT Tanzania yenye alama 19, inashika nafasi ya 8 inaweza kusogea hadi nafasi ya 6 kama itaibuka na ushindi