Msuva, Wydad bado hakijaeleweka

Joel JJ By Joel JJ β€’ 24th December 2024

Msuva, Wydad bado hakijaeleweka

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga Al Talaba ya Iraq, Simon Msuva amesema bado hajaingiziwa pesa zozote kutoka Wydad AC anazowadai

Msuva aliishtaki Wydad Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kutokana na kushindwa kumlipa pesa za usajili ikiwemo malimbikizo ya mshahara Dola 700,000 sawa na zaidi ya Sh1.6 bilioni

Msuva amethibitisha kuwa bado anaendelea kusubiri kwani hadi sasa bado hajaingiziwa fedha hizo

"Sina mengi ya kukuelezea lakini tuendelee kusubiri hadi sasa sijalipwa pesa yangu, hivyo Wydad imefungiwa kusajili wachezaji wa ndani ya Morocco na nje ya kimataifa hadi watakaponilipa pesa zangu," Msuva alinukuliwa na Mwanaspoti

Julai 2022, Mshambuliaji huyo aliishtaki Wydad kwa kosa la kuvunja mkataba kinyume na utaratibu baada ya kuwa katika mvutano wa kimasilahi na vigogo hao wa soka la Afrika ambao walimsajili Novemba 2020 akitokea Difaa El Jadida ya Morocco

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’