Local,Normal News,Azam, Simba

Ahoua, Fei Toto wachuana mabao ya penalti

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Dec 2024
Ahoua, Fei Toto wachuana mabao ya penalti

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Jean Ahoua na Feisal Salum 'Fei Toto' wa Azam FC, wanaongoza kwa kufunga mabao ya penalti katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu inayoendelea

Wachezaji hao wamefunga mabao matatu kwa njia hiyo, wakiwa hawajapoteza hata penalti moja waliyopewa dhamana ya kupiga

Ahoua alitimiza bao la tatu kwa njia ya tuta alipofunga na kuipa Simba ushindi wa bao pekee katika mechi dhidi ya JKT Tanzania iliyochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam juzi

"Hii siyo ya kwangu peke yangu, ni ushindi wa timu nzima, kila mmoja amechangia kupata ushindi, nafikiri tufurahi leo (juzi), tumepata pointi tatu, tutaangalia mechi ijayo," alisema Ahoua

Rekodi zinaonyesha kiungo mshambuliaji huyo ambaye ni raia wa Ivory Coast, alifunga mabao mengine ya penalti dhidi ya Dodoma Jiji, Simba ikishinda pia bao 1-0, nyingine dhidi ya KMC, akiiwezesha timu yake kushinda mabao 4-0

Amepachika jumla ya mabao 7 akiwa nyuma ya kinara wa mabao Elvis Rupia kwa tofauti ya bao 1 tu

Kwa upande wa Fei Toto, penalti zake alizifunga katika mchezo kati ya Azam FC dhidi ya KenGold, ikishinda mabao 4-1, dhidi ya Kagera Sugar ikiipa timu yake ushindi wa bao 1-0, na dhidi ya Dodoma Jiji, Wanalambalamba wakishinda mabao 3-1

Wachezaji wanaofuatia kwa kufunga mabao mengi ya penalti ni, Leonel Ateba wa Simba, Erasto Nyoni wa Namungo na Morice Chukwu wa Tabora United. Ateba alifunga katika mechi ambayo Simba ilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Coastal Union, na Pamba Jiji likiwa ni bao pekee kwenye mchezo huo

Morice alifunga penalti zake kwenye mchezo ambao Tabora United ilishinda bao 1-0 dhidi ya Pamba Jiji na dhidi ya Mashujaa, ikishinda pia bao 1-0

Aidha, Fei Toto ndiye kinara wa 'asisti' mpaka sasa kwenye Ligi Kuu, akiwa ametoa pasi saba za mwisho. Kiungo mshambiliaji huyo anafuatiwa na Salum Kihimbwa wa Fountain Gate FC ambaye ana 'asisti' tano, huku Ahoua, Josephat Bada wa Singida Black Stars wote wakiwa na 'asisti' nne, pamoja na Stephane Aziz Ki wa Yanga

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’