Mpepo anukia Tabora United

Joel JJ By Joel JJ β€’ 7th January 2025


Mpepo anukia Tabora United

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa akikipiga kunako ligi kuu ya nchini Zambia, Eliuter Mpepo , yuko mbioni kusaini mkataba kujiunga na Tabora United

Mbali na Tabora, mchezaji huyo amegeuka lulu kwenye Ligi Kuu ya NBC baada vilabu vingine kuingilia dili hilo wakiitaka saini yake

Mpepo amewahi kukipiga Mtibwa Sugar, Prisons, Singida United, Build Con na Trident zote za Zambia na Interclube ya Angola

Waajiri wake wa zamani, Tz Prisons wao wameenda mbali zaidi na tayari wapo kwenye mazungumzo na nyota huyo ili kuweza kuinasa saini yake


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.