Kiungo mshambuliaji wa Yanga Clatous Chama amerejea katika timu hiyo baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani wiki tatu
Chama aliumia kiwiko cha mkono katika mchezo wa raundi ya tatu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe uliopigwa Lubumbashi na kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha urejeo wa Chama ambaye ameanza mazoezi na wachezaji wenzake
Hata hivyo Kamwe amesema Yanga itaendelea kuwakosa Yao Kouassi, Maxi Nzengeli na Aziz Andambwile ambao bado wanauguza majeraha
Nyota hao wataukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Al Hilal utakaopigwa Jumapili, Januari 12 huko Mauritania
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka nchini Alfajiri ya Alhamisi kuelekea Mauritania