International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Januari 09 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Jan 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Januari 09 2025

Manchester United wamefikia mkataba mpya na Amad Diallo, Kobbie Mainoo na Alejandro Garnacho kusalia Old Trafford, Arsenal wanalenga kumnunua Bryan Mbeumo msimu huu

Winga wa Ivory Coast Amad Diallo, 22, amekubali masharti ya mkataba mpya na Manchester United. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 19, na winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, wote bado wana nafasi ya kuendelea kusalia Manchester United, licha ya wasiwasi wa kukiuka sheria za faida na uendelevu (PSR). (Sky Sports)

Manchester United inahitaji kufanya mauzo ili kufadhili uhamisho wa euro 60m (£50m) wa mlinzi wa Ureno na Paris St-Germain Nuno Mendes, 22. (Independent)

Mshambuliaji wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo, 25, yuko kwenye orodha ya wachezaji wanaowania uhamisho wa majira ya joto. (Florian Plettenberg)

Vilabu vya Ujerumani Bayer Leverkusen, RB Leipzig, Mainz, Borussia Dortmund na Stuttgart zote zinamwinda kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza James McAtee, 22. (Telegraph - usajili unahitajika)

Manchester City bado wanamtaka Omar Marmoush, 25, mwenye thamani ya pauni milioni 50, lakini huenda wakapata shida kumzawadia mshambuliaji huyo wa Misri kutoka Eintracht Frankfurt mwezi Januari huku klabu hiyo ya Ujerumani ikipigania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa. (Guardian)

Man City pia wanafikiria kumnunua beki wa Nottingham Forest na Nigeria Ola Aina, 28. (GiveMeSport) Manchester United wana habari kuwa wawakilishi wa mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, wanafanya mazungumzo na AC Milan. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo anataka kuungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United Casemiro, 32, na ameomba klabu ya Al-Nassr kumnunua kiungo huyo wa Brazil. (Mirror)

Manchester City wamepiga haua katika mazungumzo ya kumsajili beki wa Uzbekistan Abdukodir Khusanov, 20. (Team Talk)

Winga wa Brazil Antony, 24, amekataa nafasi ya kujiunga na klabu ya Ugiriki ya Olympiakos lakini bado anataka kuondoka Manchester United. (Mirror)

West Ham wanavutiwa na kiungo wa Uingereza Kiernan Dewsbury-Hall, 26, na huenda wakashinikiza mkataba wa mkopo na Chelsea. (Independent)

Inter Milan wanaandaa ofa ya kumnunua mlinzi wa Ukraine na Arsenal Oleksandr Zinchenko, 28. (Sun)

Aston Villa inamfuatilia winga wa Borussia Dortmund Muingereza Jamie Jermaine Bynoe-Gittens, 20. (Caught Offside)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’