Tanzania Prisons imeendelea kujiimarisha kuelekea mzunguuko wa pili ligi kuu ya NBC ambapo maafande hao wamefanikiwa kunasa nyota wawili kwa mkopo kutoka klabu ya Singida Black Stars
Kiungo wa ushambuliaji Rabbin Sanga ametua Tanzania Prisons kwa mkopo wa miezi sita akitokea Singida Black Stars
Rabbin aliwahi kuitumikia Fountain Gates katika timu za vijana na timu kubwa
Prisons pia imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji Amade Momade (28) kwa mkopo wa miezi sita. Momade ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Msumbiji



