Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya CAF msimu huu Yanga na Simba leo wamesafiri nje ya nchi kusaka alama muhimu katika michuano ya ligi ya mabingwa (CAF CL) na kombe la Shirikisho (CAF CC)
Yanga inakabiliwa na mechi ngumu huko Mauritania kuwania alama tatu mbele ya Al Hilal katika mchezo ambao unaweza kuamua hatma ya Wananchi katika kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo utakaopigwa Jumapili, Januari 12 ili kuweka hai matumaini ya kufuzu robo fainali
Watani zao Simba wao wameelekea Angola kuikabili Bravos Fc katika mchezo wa kombe la Shirikisho utakaopigwa Jumapili, Januari 12
Simba inahitaji ushindi au sare ili kufuzu robo fainali mapema