International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Januari 10 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Jan 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Januari 10 2025

Manchester United iko tayari kuchuana na Paris St-Germain kumnunua mshambuliajii wa Napoli na Georgia Khvitcha Kvaratskhelia, 23. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Liverpool pia wana nia ya kumnunua Kvaratskhelia ikiwa Napoli itamruhusu kuondoka mwezi huu. (Athletic)

West Ham wanamfuatilia mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford na wanataka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa mkopo kutoka Manchester United. (Talksport)

Vilabu vya Serie A AC Milan na Como pia vina nia ya kumsajili Marcus Rashford kwa kipindi kilichosalia cha msimu huu. (Gianluca Di Marzio)

Nyota wanne wa Bournemouth wanavutia vilabu vikuu vya Ligi ya Premia, huku Illia Zabarnyi, Milos Kerkez, Antoine Semenyo na Dean Huijsen wakifuatiliwa na Chelsea, Newcastle na Liverpool.

Manchester United wameungana na Arsenal katika mbio za kumnunua mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo, 25, kutoka Brentford. (Mirror)

Manchester City wanafanyia kazi mpango wa kumsajili beki wa Brazil mwenye umri wa miaka 18 Vitor Reis kutoka Palmeiras. (Athletic)

Nottingham Forest wamemuulizia mchezaji wa Juventus Douglas Luiz, 26, lakini kiungo huyo wa kati wa Brazil yuko anawaniwa Manchester United, Manchester City na Fulham. (Mail)

Kipa wa Southampton na England Aaron Ramsdale, 26, anafuatiliwa na Newcastle. (Sun)

Borussia Dortmund wamemtafuta mlinzi wa Manchester City mwenye umri wa miaka 19 Max Alleyne. (Fabrizio Romano) Kiungo wa kati wa Liverpool na England Harvey Elliott, 21, ananyatiwa na klabu za Brighton na Borussia Dortmund. (Lyall Thomas)

Tyrick Mitchell wa Crystal Palace, 25, anasakwa na vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ya England na beki huyo pia amekuwa akiwindwa na Atletico Madrid. (Mirror)

Aston Villa wanajadiliana na klabu ya Ligue 2 Caen kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Tidiam Gomis, 18. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Juventus wamemfanya beki wa kati wa Barcelona Ronald Araujo, 25, kuwa lengo lao kuu huku wakilenga kusajili beki mpya mwezi huu. (Fabrizio Romano)

Fulham wamepokea ofa iliyoboreshwa ya £20.5m kutoka Palmeiras kwa kiungo wa kati wa Brazil Andreas Pereira, 29. (Mail)

West Ham wamepewa fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Canada na Lille Jonathan David mwenye umri wa miaka 24. (GiveMeSport)

Bournemouth wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Paraguay mwenye umri wa miaka 29 na LDU Quito Alex Arce kwa mkopo. (Football Insider)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’