Napoli wanatarajiwa kuwasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Muingereza Marcus Rashford, 27, huku winga wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia akitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Italia. (Mirror)
Paris St-Germain wanakaribia kumsajili Kvaratskhelia kutoka Napoli, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 tayari ameshakubali mkataba na timu hiyo ya Ufaransa. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)
PSG wanaamini kuwa wanaweza kuwashawishi Aston Villa kuwauzia mshambuliaji wa Colombia Jhon Duran, 21, na klabu hiyo ya Ligue 1 ina nia ya kumjumuisha mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, katika mazungumzo yoyote. (Mail)
Kiungo mshambulizi wa Uhispania Marco Asensio, 28, anatarajiwa kuhama PSG, huku Aston Villa, Juventus na Real Sociedad wakitarajiwa kuwa mojawapo wa klabu anazoweza kujiunga nazo. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)
Barcelona wanamtaka mshambuliaji wa Newcastle United Alexander Isak na wanaweza kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 mwezi Januari au msimu wa joto, kulingana na hali yao ya kifedha. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
AC Milan wana nia ya kumsajili beki wa Uingereza Kyle Walker, huku meneja wa Manchester City Pep Guardiola akisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 aliomba kuondoka katika klabu hiyo ya Uingereza. (Guardian)
BBC