Hatma ya Yanga mikononi mwa Al Hilal CAF CL leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 12th January 2025


Hatma ya Yanga mikononi mwa Al Hilal CAF CL leo

Mechi za raundi ya tano hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika zinaendelea kutimua vumbi leo Jumapili ambapo mabingwa wa Tanzania Bara Yanga wako ugenini kumenyana na Al Hilal huko Mauritania

Dakika za mchezo huo utakaopigwa saa 4 usiku zitaamua hatma ya Yanga kuendelea kuwania tiketi ya robo fainali au kuyaaga mashindano hayo

Leo Yanga inahitaji ushindi au hata matokeo ya sare ili kuendelea kubaki na matumaini ya kusonga mbele lakini kama itapoteza mchezo huo, basi itaaga rasmi mashindano

Al Hilal inayoongoza kundi A ikiwa na alama 10 tayari imekata tiketi ya robo fainali lakini katika mchezo huo inahitaji angalau alama 1 ili kujihakikishia kumaliza nafasi ya kwanza katika kundi

MC Alger itakuwa ikifuatilia kwa karibu mchezo huo kwani matokeo ya ushindi kwa Al Hilal yatawapa tiketi ya kutinga robo fainali na alama zao nane

Endapo Yanga itashinda itafikisha alama 7 na ili kufuzu itahitaji kushinda mechi ya mwisho dhidi ya MC Alger ambayo itapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Januari 18

Lakini pia kama Yanga itapata sare leo, itakuwa bado na nafasi ya kutinga robo fainali kama itashinda kuanzia mabao 2-0 katika mchezo dhidi ya MC Alger


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.