Simba yafuzu robo fainali CAF CC

Joel JJ By Joel JJ β€’ 12th January 2025


Simba yafuzu robo fainali CAF CC

Simba imefanikiwa kutinga robo fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC) baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Bravos Fc katika mchezo uliopigwa huko Angola

Makosa ya beki Che Malone Fondoh yaliinufaisha Bravos kufunga bao la mapema hata hivyo Lionel Ateba aliisawzishia Simba katika kipindi cha pili bao ambalo limeihakikishia Simba kufuzu

Pengine ulikuwa mchezo ambao Simba ingeweza kuibuka na ushindi Kibu Denis akikosa nafasi tatu katika kipindi cha kwanza

Ulikuwa mchezo ambao Simba iliucheza kimkakati zaidi na hatimaye mpango wa kocha Fadlu Davids umekamilika


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.