Mauya kuibukia Ken Gold

Joel JJ By Joel JJ β€’ 13th January 2025


Mauya kuibukia Ken Gold

Klabu ya KenGold iko katika hatua ya mwisho kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji Zawadi Mauya kutoka klabu ya Singida Black Stars, imefahamika

Mazungumzo baina ya vilabu vya Singida Black Stars na Ken Gold juu ya mchezaji huyo yapo katika hatua za mwisho

Muda wowote kuanzia sasa usajili huo utakamilika, Mkataba wa Miezi Sita wa kuwatumikia Ken Gold pia wenye kipengele cha kuongeza zaidi endapo wataridhia huduma yake kwa msimu ujao

Mauya alijiunga na Singida BS msimu huu akitokea klabu ya Yanga aliyoitumikia kwa misimu minne

Hata hivyo kiungo wa zamani wa Kagera Sugar amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Singida BS


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.