Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, Januari 14 2025

Joel JJ By Joel JJ β€’ 14th January 2025


Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, Januari 14 2025

Manchester United wanasemekana kumthamini winga Alejandro Garnacho, 20, kwa takribani pauni milioni 42, huku kukiwa na nia ya Napoli kumnyakua mchezaji huyo (Sport Italia)

Bayern Munich wameungana na Chelsea katika mbio za kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Uingereza Kobbie Mainoo, 19. (Sun)

Manchester City wako tayari kumruhusu mlinzi Kyle Walker, 34, kuondoka bila malipo mwezi huu huku AC Milan na Inter Milan wakionesha nia ya kumnasa mchezaji huyo. (Gazzetta dello Sport, nje)

AC Milan itamfuatilia rasmi mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 27, ambaye anatazamiwa kuondoka Old Trafford mwezi huu. (Sky Sports)

Borussia Dortmund pia wameripotiwa kukutana na wawakilishi wa Rashford kwa matumaini ya kufikia mkataba wa Januari. (Sky Sport Ujerumani)

Aston Villa wamekubali mkataba wa pauni milioni 19 kumsaini mshambuliaji wa Uholanzi Donyell Malen, 25, kutoka Borussia Dortmund. (Athletic)

Villa pia wameanzisha mazungumzo na Sevilla huku wakitafuta kumsajili beki wa Ufaransa Loic Bade mwenye umri wa miaka 24. (L'Equipe)

Leicester wanajiandaa kumsajili mlinzi wa pembeni wa Ufaransa Woyo Coulibaly, 25, kutoka Parma kwa mkataba wa pauni milioni 3. (Fabrizio Romano)

Chelsea itamruhusu kiungo Carney Chukwuemeka, 21, kuondoka kwa mkopo mwezi huu, huku Borussia Dortmund na Strasbourg zikimuwania. (Fabrizio Romano)

Nottingham Forest iko tayari kupokea ofa kwa ajili mshambuliaji Emmanuel Dennis, 27, klabu zenye nia zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa, Serie A na La Liga. (Sky Sports)

Beki wa Ureno Renato Veiga, 21, ana uwezekano wa kuondoka Chelsea mwezi Januari, huku klabu za Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Italia zikionesha nia ya kumpata. (Athletic)

Monaco wametoa pendekezo la pili kwa West Ham kwa ajili ya Edson Alvarez, 27, baada ya ofa yao ya awali ya mkopo kwa kiungo huyo wa Mexico kugonga mwamba. (Mail)

Beki wa Uholanzi Tyrell Malacia, 25, anaweza kuondoka Manchester United kwa mkataba wa mkopo mwezi huu. (Fabrizio Romano)

Real Madrid wanaangalia uwezekano wa kuchagua wasimamizi kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti baada ya kufungwa 5-2 na Barcelona kwenye fainali ya Spanish Super Cup. (Relevo)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.