Dirisha dogo la usajili lilifungwa usiku wa kuamkia leo huku Yanga ikitangaza kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Jonathan Ikangalombo
Ikangalombo (22) ametua Yanga akitokea klabu ya AS Vita ambapo winga huyo amesaini mkataba wa miaka 2
Nyota huyo ametua Yanga akichukua nafasi ya Mcongomani mwenzake Jean Baleke ambaye timu hiyo imemrejesha kunako klabu yake ya TP Mazembe
Baleke alijiunga na Yanga kwa mkopo katika dirisha kubwa lakini alishindwa kumshawishi aliyekuwa kocha wa Yanga Miguel Gamondi na kocha wa sasa Sead Ramovic
Katika dirisha dogo Yanga imesajili wachezaji wawili, Israel Mwenda na Ikangalombo