Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amewataka Wanasimba kuheshimu adhabu iliyotolewa na CAF kwa kuhakikisha hawafiki uwanja wa Benjamin Mkapa wakati mchezo kati ya Simba dhidi ya CS Constantine utakapopigwa siku ya Jumapili
Ahmed amesema CAF wametoa masharti ambayo klabu ya Simba inapaswa kuyatekeleza ili kuepuka kukumbana na adhabu kubwa
Aidha Simba imeandaa eneo maalum ambapo mashabiki wa jijini Dar es salaam wanaweza kujumuika kushuhudia mchezo huo
"Tuna kazi kubwa ya kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi letu. Kama mnavyojua mchezo wetu tumezuiliwa kuingiza mashabiki kuingia uwanjani. Limekuwa tukio la kuumiza sana na wengine mpaka sasa bado hawajaamini, imetuchanganya pakubwa"
"Adhabu hii ni mechi moja ambapo tukitumikia adhabu hii vizuri mechi ya robo fainali mashabiki wataingia uwanjani. Niwambe Wanasimba tuheshimu hii adhabu, mtu yoyote hata kama ni mjanja kiasi gani wa kuingia uwanjani, niwaombe Wanasimba kukaa mbali na Uwanja wa Mkapa"
"Kuna watu ambao watakuwa wanaangalia kama tumefata utaratibu. Tuna idadi maalumu ya watu kuingia uwanjani hivyo hatazidi mtu hata mmoja. Kuna utaratibu tumepewa na CAF na sisi Simba tutaufata utaratibu huo"
"Kumekuwa na maoni mengi watu wakitaka tuweke screen kubwa kwenye uwanja wa Uhuru ili kelele zitakazopigwa ziwafikie wachezaji. Hairusiwi watu kukaa mita 1,000 kutoka uwanja wa Mkapa. Jambo hilo haliwezekani na kufanya hivyo ni kuvunja sheria"
"Asiyehusika yoyote akae mbali na Uwanja wa Mkapa, najua tunaumia hata mimi mwenyewe naumia. Kwa kuwa watu wanataka kuiona timu yao pamoja kama tulivyozoea, mdhamini wetu wa michuano ya kimataifa akaona atuandalie kitu cha kutuweka pamoja"
"Mo Cola ametutengea eneo maalumu la kukutana kuona timu yetu na eneo lenyewe ni Mwembe Yanga lililopo Temeke. Tutakuwepo pale kuanzia saa 5 asubuhi na kutakuwa na screen kubwa vibaya mno, hamjawahi kuiona"
"Kutakuwepo na burudani mbalimbali siku hiyo kama mwimbaji wa nyimbo ya Wivu ambaye ni Dj Mushizo lakini pia atakuwepo Dj Sinyorita"
"Lakini pia wiki mbili ziliopita tulizindua kampeni ya Onja na Ushinde ukinywa Mo Cola. Hivyo siku ya Jumapili Januari 19, 2025 kutakuwa na zoezi la kugawa zawadi kwa washindi na wengine watashinda pale pale"
"Mimi binafsi Jumapili sitaenda uwanjani, taenda Mwembe Yanga. Nimeshazoea kelele hivyo takuwa na Wanasimba wenzangu kufurahia," alisema Ahmed