Safari ya Yanga katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu imefika tamati leo baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya MC Alger katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga ilihitaji kushinda leo ili kufuzu robo fainali lakini jitihada ndani ya dakika 90 hazikutosha kuwapa Wananchi alama zote tatu
MC Alger walijilinda vyema huku mbinu yao ya kupoteza muda ikiwabeba katika mchezo ambao pengine Yanga ingeweza kushinda ikipoteza nafasi adimu katika kipindi cha pili
Unaweza sema safari ya Yanga katika ligi ya mabingwa msimu huu iliharibika mapema baada ya kukubali kupoteza mechi mbili za kwanza dhidi ya Al Hilal na MC Alger
Sio matokeo ambayo wengi waliyatarajia lakini ndio mpira miguu, Yanga inapaswa kujipanga kuhakikisha inarejea katika michuano hiyo msimu ujao ikiwa na nguvu kubwa zaidi



