Kikosi cha Simba jioni ya leo kitashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili CS Constantine katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho (CAF CC)
Ni mechi ya kuilinda heshima ya Tanzania katika mashindano ya CAF, Simba ikiwa klabu pekee iliyofuzu robo fainali msimu huu
Hesabu za vijana wa kocha Fadlu Davids ni kushinda mchezo huo ili kuhakikisha wanakwenda kileleni mwa kundi A ili kupata droo rafiki katika hatua ya robo fainali
Kama Simba itamaliza nafasi ya kwanza kundi A itaanzia ugenini na kumalizia nyumbani mechi ya robo fainali
Lakini pia Mnyama atacheza dhidi ya timu iliyomaliza nafasi ya pili katika kundi jingine na hivyo kukwepa vigogo wengine watakaomaliza nafasi ya kwanza
Ni bahati mbaya kwa mashabiki mechi hiyo wataishuhudia kwenye TV kutokana na adhabu ya kufungiwa mechi moja ambayo Simba wamekumbana nayo kutoka CAF
Ni pigo kwa upande wa mashabiki lakini halitakuwa pigo kwa kikosi cha Simba kwani mechi mbili zilizopita, imepata matokeo mazuri ugenini katika mechi ambazo hakukuwa na mashabiki
Walishinda bao 1-0 Tunisia dhidi ya CS Sfaxien na kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Bravos nchini Angola



