Mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize ameibuka mchezaji bora wa mwezi Disemba 2024 Ligi Kuu ya NBC huku kocha Sead Ramovic akibeba tuzo ya kocha bora katika mwezi huo
Mzize alishinda tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango bora Disemba akifunga mabao manne na kutoa pasi tatu za mabao
Mzize aliwashinda Prince Dube wa Yanga na Feisal Salum wa Azam Fc
Kwa upande wa tuzo ya kocha bora, Ramovic ameibuka kidedea mbele ya Fadlu Davids wa Simba na Rachid Taoussi wa Azam Fc baada ya kuingoza Yanga kushinda mechi zote

