Msemaji wa Singida Black Stars Hassan Masanza amethibitisha kuna baadhi ya wachezaji wao wa kigeni wameomba uraia wa Tanzania lakini klabu hiyo haijahusika kuwashawishi na kuwa wamechukua maamuzi hayo kwa utashi wao
Jana zilisambaa taarifa kuhusu wachezaji Emmanuel Keyekeh (27) raia wa Ghana, Arthur Bada (22) raia wa Ivory Coast, Amas Obasogie (22) raia wa Nigeria na Damaro Camara (21) raia wa Guinea kupewa uraia wa Tanzania baada ya kukamilisha taratibu zote za Uhamiaji
Masanza amesema Singida BS haina mamlaka ya kubadili uraia wa mchezaji, kama klabu iliwapa ushirikiano wachezaji hao katika kukamilisha adhma yao ya kuwa Watanzania
"Ni kweli, baadhi ya wachezaji wetu wameomba uraia wa Tanzania kwa ridhaa yao, jambo limeenda vizuri na limekamilika. Sisi hatuna mamlaka ya kumbadilishia mchezaji uraia, wao walionyesha nia, walifuata taratibu za mamlaka husika na sisi tukawasapoti," alisema Masanza
Taarifa zaidi imebainisha kuwa TFF inakusudia kuwajumuisha nyota hao katika kikosi cha timu ya Taifa kitakachoshiriki michuano ya CHAN na Afcon baadae mwaka huu
Idara ya Uhamiaji ya Tanzania yathibitisha kuwatunuku Uraia wa Tanzania wachezaji 3 wa Singida Black Stars kutoka Ghana, Guinea na Ivory Coast. pic.twitter.com/qMjHWZw9Cm
— Bin Kazumari (@jemedarisaid) January 23, 2025