Local,Transfer News,Kagera, Pamba

Mpole apewa jukumu la kuibeba Kagera Sugar

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Jan 2025
Mpole apewa jukumu la kuibeba Kagera Sugar

Kocha wa Kagera Sugar, Melis Medo ameonyesha imani kubwa kwa mshambuliaji mpya, George Mpole, akisema ana uwezo wa kufanya mambo makubwa na kuwa msaada katika juhudi zao za kujinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka Ligi Kuu Bara

Medo amesema kwamba Mpole atakuwa silaha muhimu katika timu hiyo hasa katika duru la pili la Ligi Kuu Bara ambapo Kagera Sugar inakutana na changamoto kubwa ya kupigania kubaki kwenye ligi

Mpole ambaye amejiunga na Kagera Sugar akitokea Pamba Jiji katika dirisha dogo lililofungwa Januari 15 ni mchezaji mwenye rekodi nzuri akiwahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara 2021/22 baada ya kufunga mabao 17

Medo alisema anaamini uzoefu wa Mpole utaongeza nguvu katika timu yake ambayo inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 11

"George Mpole ni mshambuliaji ambaye ana uzoefu mkubwa na amewahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara. Ana uwezo wa kuleta madhara makubwa katika maeneo muhimu uwanjani. Hii ni silaha muhimu kwa timu yetu kwani tunahitaji mchezaji ambaye anaweza kuleta ubunifu mbele na kumalizia nafasi za kufunga" 

"Tunahitaji wachezaji kama yeye ambao hawana hofu wanapambana hadi dakika ya mwisho na wanajua jinsi ya kutumia nafasi. Huu ndio ubora tunaohitaji ili kujinasua katika nafasi tuliyopo sasa,” alisema Medo

Mbali na Mpole, Kagera Sugar pia imetambulisha nyota mwingine katika dirisha lililofungwa la usajili ambaye ni kipa Ahmed Feruzi aliyejiunga kwa mkopo akitokea Simba, na Medo anaamini kuwa kuongezwa kwa kipa huyo kutaimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo

Mwanaspoti

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
59m ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
11h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
18h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’