Yanga kumaliza hasira kwa Copco?

Joel JJ By Joel JJ β€’ 23rd January 2025


Yanga kumaliza hasira kwa Copco?

Baada ya mapumziko ya siku chache, kikosi cha Yanga jana kilirejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho la CRDB hatua ya 64 bora dhidi ya Copco Fc

Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Januari 25 katika uwanja wa KMC Complex

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema baada ya kuondoshwa katika michuano ya ligi ya mabingwa, wanapaswa kukusanya nguvu ili kuhakikisha wanatetea mataji yao yote

Kamwe amesema kama watashindwa kutetea taji la Ligi Kuu na FA, maumivu yake yatakuwa makubwa kuliko maumivu waliyopata baada ya kushindwa kufuzu robo fainali CAF CL

"Tumerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa kombe la FA dhidi ya Copco ambao utapigwa Jumamosi uwanja wa KMC Complex"

"Mchezo huu unaonekana kama mwepesi lakini sio kweli kwani tunahitaji kufanya kazi ya ziada, tumetoka kwenye huzuni ya kushindwa kufuzu robo fainali ya CAF CL"

"Kama hatutauchukulia mchezo huu kwa umakini, mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi kwetu"

"Tuna jukumu la kutetea mataji yetu yote tukianza na hili la FA. Kama tutashindwa kutetea makombe haya basi maumivu tutakayopata ni makubwa pengine kuliko tuliyopata baada ya kushindwa kufuzu robo fainali CAF CL," alisema Kamwe


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.